,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, June 26, 2017

BAADA ya hivi karibuni mkongwe wa filamu Bongo, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ kudaiwa kuwadhalilisha wasanii wa kike anaofanya nao tamthiliya huko Lushoto, Tanga na kusababisha kamati kuundwa kwa ajili ya kuchunguza hilo, bado suala hilo ni pasua kichwa kwa wahusika


Akizungumza na Wikienda, mwenyekiti wa kamati hiyo iliyoundwa na Chama cha Waigizaji Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ alisema kuwa suala hilo ni zito hivyo kutokana na uzito huo wamepanga siku kumi na nne kwa ajili ya uchunguzi na kupata ukweli.

“Unajua hili suala ni zito sana tofauti na watu wanavyolichukulia, kwa sasa bado tunaendelea na uchunguzi, hatuwezi kusema kinachoendelea maana tutaharibu uchunguzi, tumekubaliana tutafanya uchunguzi kwa siku kumi na nne na ripoti ya uchunguzi itatolewa na siyo kwa Chuz tu bali kwa wasanii wote wenye tabia hizo,” alisema Mike.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi