,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, June 25, 2017

Bango lenye kuonyesha Mtaa wa Victor Wanyamamchezaji mashuhuri wa soka katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ambao ulipewa jina lake jana na Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob, limeng’olewa leo na wananchi wakipinga kwamba utaratibu wa kuupa mtaa huo jina hilo haukufuatwa.

Wakati huohuo, Kitengo cha Habari na Uhusiano cha Halmashauri ya Manispaa ya Ubungok imetoa ufafanuzi kuhusu kile kilichoita makosa yaliyofanywa na viongozi wa kata ya Ubungo katika kuupa mtaa huo jina la Mkenya huyo.


UFAFANUZI KUHUSU MAKOSA YALIYOFANYWA NA VIONGOZI WA KATA YA UBUNGO KUMPA MTAA VICTOR WANYAMA
Majina ya mitaa hupendekezwa na kamati za mitaa husika kisha hupelekwa kwenye vikao vya WDC vya kata halafu maamuzi ya WDC hupelekwa kwa Mkurugenzi kwa ajili ya kuingizwa kwenye kikao Cha kamati ya Fedha na uongozi, Baraza la Madiwani, halafu DCC, RCC na Kisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na baadaye kwa Mchapaji mkuu wa serikali na mwisho hutokea kwenye Tangazo la serikali GN.
Na hapo ndipo mtaa hujulikana huo ni mtaa fulani. Taratibu za kubadili pia lazima zifuate hatua hizo muhimu.

KILICHOFANYIKA NI KINYUME NA UTARATIBU WA KISHERIA
Imetolewa Na; 
Kitengo Cha Habari na Uhusiano 
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
0 comments:

Post a Comment

ufunguzi