,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, July 27, 2017Dua kwa ajili ya mke mdogo (wa pili) wa Alhaj Mzee Yussuf aliyefariki dunia Juni 18, mwaka huu, Chiku Khamis, iliyokuwa ifanyike Jumapili iliyopita nyumbani kwao Kariakoo jijini Dar es Salaam, haikufanyika kama ilivyotarajiwa na hivyo kuzua utata.
Siku chache baada ya shughuli za mazishi kumalizika, dada wa marehemu Chiku aitwaye Amina, aliwaambia waandishi kuwa dua kwa ajili ya ndugu yao ingefanyika Julai 23, mwaka huu, siku ambayo familia zote mbili zingekutana na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayowahusu wanandugu wa pande hizo.
Hata hivyo, wiki mbili zilizopita kulitokea sintofahamu baada ya kudaiwa kuwa Mzee Yusuf alichukua nguo za marehemu mkewe, zilizokuwa katika nyumba aliyokuwa akiishi huko Chanika na kuzipeleka Kariakoo kwa ndugu zake, kitendo ambacho kiliwachukiza ndugu wa mwanamke, kiasi cha kutokea kutoelewana kati yao na Mzee Yusuf.
Hoja ya ndugu wa marehemu Chiku, ilikuwa kwamba halikuwa jambo sahihi kwa Mzee Yusuf kuchukua nguo hizo bila ya uwepo wa ndugu wa marehemu, kwani huenda kulikuwa na siri za kike ambazo hakupaswa kuzijua.
Chanzo makini kilicho karibu na familia hiyo, kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa inavyoonekana bado kuna mgogoro wa chinichini kati ya Mzee Yusuf na ndugu wa Chiku kwani siku ambayo ilipangwa kufanyika kwa dua hiyo haikufanyika na hazikutolewa sababu zozote.
Risasi Mchanganyiko lilifika nyumbani kwa akina Chiku Kariakoo Jumapili iliyopita, lakini hakukuwa na dalili zozote za kufanyika kwa jambo hilo, kwani eneo lote lilikuwa kimya.
Mmoja wa wanandugu, kijana ambaye alidai ni mdogo wa marehemu, aliyekataa kutaja jina lake, alisema hafahamu ni lini shughuli hiyo itafanyika na wala hajui kama kuna kitu kama hicho. Dada wa marehemu Chiku, Amina hakupokea simu yake ya mkononi kwani muda wote iliita bila kupokelewa.
Lakini alipopatikana mume wa marehemu, Mzee Yusuf na kuulizwa kuhusu kutofanyika kwa shughuli hiyo kama ilivyotangazwa awali, alisema kwa mkato; “Sijajua chochote mimi mpaka sasa hivi na kuhusu kufanya 40 huo mpango nitajua mwenyewe.”

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi