,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, July 10, 2017

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amesalimu amri na kutangaza kurejesha serikalini (TRA) fedha za mgawo wa Escrow kiasi cha milioni 40.4 kama sehemu ya mgao aliokuwa amepewa na Mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira

Ngeleja amesema ingawa alipewa fedha hizo kama sehemu ya msaada , ameamua kurudisha fedha hizo ili kukwepa kashfa hiyo ya ESCROW
"Fedha hizo nilizipokea kwa nia njema kama msaada kutoka kwa ndugu yangu Rugemalira ili zinisaidie katika majukumu yangu ya kibunge na kutekeleza shughuli za kijamii kama vile ujenzi wa makanisa, misikiti na kulipia karo za wanafunzi na vile vile nilipokea fedha hizo ili zinisaidie katika kutekeleza shughuli za kibunge ambazo hazipo katika bajeti ya serikali". Amesema Ngeleja mbunge wa Sengerema
Akizidi kuelezea sababu za kurudisha fedha, Mbunge huyo amesema
"Nilipokea Fedha hizo bila kujua kwamba fedha hizo zilikuwa zinahusishwa na kashfa ya akaunti ya fedha za Escrow kama ilivyo sasa, Nilipokea msaada huu kama wapokeavyo wabunge wengine, kwa nia njema. Nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha kiasi cha Milioni 40.4 serikalini (TRA)". Ameongezea Ngeleja
Mbunge huyo alipewa mgao huo wa fedha kiasi cha milioni 40.4 na Ndugu James Rugemalira kupitia benki ya Mkombozi mnamo tarehe 12 februari 2014 na jambo hili lilimfanya mmoja wa watuhumiwa waliokula fedha za mgao wa ESCROW

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi