,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, July 31, 2017

Image result for fatma karume images


*Amfokea Hakimu Kisutu wakati akiendesha kesi
*Ainuka kumvaa, wasikiliza kesi, karani wamzuia

Na Rabia BakariKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, binti wa Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, Bi Fatma Karume, amemtishia kwa maneno makali huku akitaka kumshambulia Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bibi Addy Lyamuya.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mahakamani hapo jana, wakati Hakimu Lyamuya akisikiliza kesi ya madai ya mtoto kati ya Bw. Sadiq Walju na Bi Saeda Hassam ambapo Bi. Fatma alikuwa akimtetea Bw. Walju.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo namba 60 ya mwaka jana, ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi, Bw. Adolf Mahay, lakini baada ya kutokea kutokuelewana na wakili huyo (Fatma), hakimu Mahay alijitoa kusikiliza .

Septemba 20 mwaka huu, kesi hiyo ilipangwa kwa Hakimu Mkazi, Bibi Euphemia Mingi na ilipofika Oktoba 8 mwaka huu, Hakimu Mingi alijitoa kusikiliza kwa kile kilichoelezwa kufokewa mahakamani na wakili Bi Fatma na kushinikizwa kujitoa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoiendesha ipasavyo.

Jana kwa mara ya kwanza, kesi hiyo ilikuwa ianze kusikilizwa na Hakimu Mkazi, Bibi Lyamuya lakini kutokana na sababu za kimahakama aliiahirisha hadi Januari 13 mwakani.

Baada ya Hakimu Lyamuya kupanga tarehe hiyo, Bi. Fatma aliipinga na kumwambia anataka kesi hiyo isikilizwe Novemba 23 mwaka huu.

Karani alimwambia Hakimu kuwa tarehe iliyopendekezwa na wakili Fatma, imejaa hivyo hakutakuwa na nafasi, ndipo wakili huyo alipopendekeza isogezwe na kusikilizwa Januari 2 mwakani.

Baada ya pendekezo hilo, Hakimu Lyamuya alimwambia wakili huyo kwamba hatakuwa na nafasi tarehe anazolamizisha, hivyo anaomba kujitoa kusikiliza kesi hiyo na badala yake apangiwe hakimu mwingine, mwenye nafasi katika siku hizo.

Kutokana na kauli hiyo, ndipo, Bi. Fatma alianza kufoka mahakamani hapo kwa sauti hali iliyozua tafrani na watu waliokuwapo kubaki wameduwaa kwa kilichokuwa kikiendelea.

"Umeniona kwa mara ya kwanza, hunijui mimi ni nani, nitakuonesha kwanza hujui kazi, nitaandika barua kwa wakuu wako wa kazi," wakili huyo alifoka kwa jazba huku akimnyooshea kidole Hakimu Lyamuya na kumfuata alipokuwa amekaa.

Hata hivyo, Bi. Fatma alizuiwa na karani wa mahakama pamoja na watu waliokuwamo mahakamani hapo, ambao walifanikiwa kudhibiti mtafaruku huo.

Akizungumzia tukio hilo, Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Bw. Sivangilwa Mwangesi alisema amepata taarifa ya tukio hilo na atalifanyia uchunguzi.

"Nimepata malalamiko ya wote wawili, yaani wakili Bi. Fatma na Hakimu Lyamuya, nitafanya uchunguzi kwani kitendo hicho ni kinyume cha sheria, zogo wala ugomvi haviruhusiwi mahakamani, hata kama umegombana na mtu msubiri nje ya mahakama si kuleta vurugu ndani ya mahakama," alisema Bw. Mwangesi.

Aidha, Hakimu Lyamuya alisema awali wakati Bi. Fatma akimtolea maneno ya vitisho, alidhani ni utani, lakini alipomwambia kuwa ataandika barua kwa wakuu wake wa kazi, ilibidi awe makini zaidi na jambo hilo.

"Nina mashahidi, maana nimejua kwamba hafanyi mzaha, shahidi wangu wa kwanza ni Bw. Jerome Msemwa, Bw. Jabiri Mkongo, Bw. Juma Magota, Bw. Derick Ngoro na watu waliokuwa mahakamani wakati kesi hiyo ikiendelea," alisema Hakimu huyo.

Source-MAjira (22/11/2007)

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi