,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, July 12, 2017

Makamu wa Rais Samia Suluhu (kulia) akisalimiana na viongozi wa SportPesa.
Makamu wa Rais Samia Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Everton dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho Alhamisi.

Akiwa uwanjani hapo, mama Samia anatarajiwa kukutana uso kwa uso na mshambuliaji Wayne Rooney ambaye ametua Everton wiki hii akitokea Manchester United.
Katika mchezo huo, mwamuzi Israel Mujuni Nkongo ndiye atachezesha mchezo huo wa kirafiki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Gulam Abbas amesema kwamba maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika na Everton wataingia nchini kesho asubuhi.
“Everton wanaingia kesho majira ya asubuhi na Alhamisi watacheza mchezo wa kirafiki na timu kutoka nchini Kenya, Gor Mahia,” alisema Tarimba.
Gor Mahia imepata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup, ikiwafunga AFC Leopards mabao 3-0.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi