,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, July 31, 2017

Cloud 112 na mkewe wa sasa, Mina Baby.

Baada ya staa wa filamu za Kibongo, Issa Mussa ‘Cloud 112’ kutinga Bongo akitokea Sweden akiwa na mke mwingine anayetambulika kwa jina la Amina ‘Mina Baby’, mkewe wa zamani Cynthia ameibuka na kufunguka mazito.


Katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda, Cynthia ambaye Cloud baada ya kutinga Bongo alikiri kwamba ameachana naye na kila mmoja ana maisha yake, alisema kuwa, hana taarifa za kuachana au kuachwa na mumewe huyo hivyo anamtaka kama kweli ndiyo hivyo basi ampe talaka kwa maandishi.

Hata hivyo, Cynthia alisema kuwa, ataendelea kumheshimu Cloud hadi atakapoingia kaburini kwa sababu alimuoa kwa heshima na hata sasa kama amemuacha basi amuache kwa heshima.
Cloud na mkewe wa zamani, Cynthia.

“Aseme tu anatapatapa ila nitaendelea kumheshimu maana alinioa kwa heshima, hatukumkera mtu wala hatukumtoa mtu machozi.

“Yeye anasema tumeachana, lakini sina taarifa hizo, kikubwa ni kwamba kutokana na kauli zake hizo silazimishi mapenzi bali ninahitaji tu anipe talaka kwa maandishi,” alisema Cynthia.

Alisema kuwa, wakati Cloud anaondoka Bongo alimuachia mtoto wao akiwa na umri wa miaka miwili na sasa ana miaka mitano, lakini hajui anaishije wala anakula nini huku akimdanganya kwamba anaenda kutibiwa nje lakini kumbe alikwenda kuoa.

“Simlaani Cloud na mkewe na wala sina kinyongo nao, hata nikikutana nao nitawasalimia kwa furaha kabisa na kwa imani yangu kila siku ninawabariki maana maisha siyo mapenzi tu, ninawaza jinsi nitakavyohitimu masomo yangu kwa sababu kwa sasa ninasoma.

Cloud na Cynthia

“Lakini yote kwa yote ninamshukuru Mungu, mwanangu anafanana sana na baba yake (Cloud) na isingekuwa ni hivyo angeweza kusema hata mengine.

“Nauheshimu sana uamuzi wake, kama amesema tumeachana maana tangu nimekua sikuwahi kumuona mama yangu akilazimisha mapenzi kwa baba yangu, lakini atambue kwamba ukiona mwanamke anakubali mwanaume aitelekeze familia, kaa naye chonjo sana,” alisema Cynthia.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi