,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, July 11, 2017

Msanii wa Bongo Flava na mtangazaji wa Choice FM, Feza Kessy
MSANII wa Bongo Flava na mtangazaji wa Choice FM, Feza Kessy,  amesema kutokana na kazi yake ya utangazaji kuna baadhi ya vyombo vya habari nchini vimekuwa havimpi sapoti yoyote.

Mwimbaji huyo amedai kuwa kabla ya kuingia katika utangazaji mambo yalikuwa tofauti na sasa  na hivyo ameviomba vyombo hivyo vya habari vitenganishe kazi yake na muziki.
“Kwa mfano mimi kuwa CMG kuna media zinaniogopa, sijui wanavyowaza wao lakini sapoti inakuwa inapungua. Ningependa ile sapoti ya muziki iendelee kama walivyokuwa wanafanya mwanzo.  Sasa hivi wamepunguza kasi  kwani kuna sehemu hata ‘interview’ nabaniwa,” ameiambia XXL ya Clouds FM na kuongeza:
“Kuna media nyingine wanacheza muziki wangu lakini kuna ‘specific media’ ambazo hata ‘interview’ nilishindwa kupata. Siwezi kuzitaja kwa sasa hivi ila wajue ‘this is business’, ni kazi yangu ‘as an individual’ wasini-judge kikampuni,” amesisitiza.
Feza Kessy kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa  ‘Kaa Kijanja’ ambao amemshirikisha rapa kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi