,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, July 27, 2017

Msanii wa RnB Bongo, Rama Dee amefafanua mstari uliyopo katika ngoma yake mpya ‘Nibebe’, ambao unasifia maumbile ya mwanamke ambaye ni mrembo.

Katika ngoma yake hiyo ambayo imeshika kasi kila kola kuna mistari inasema, “Kalio lako ndio hatari, umenishika mahali”.
“Nimejaribu kuongea kitu ambacho kinazungumzwa kila wakati, sidhani kama kalio ni neno kali, kila mtu ana kalio ila kuna kalio ambalo linakua beautiful zaidi,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa mstari huo ameutumia kwa mtu wake wa karibu (mpenzi) na mtu yeyote anaweza kufanya hivyo iwapo atapenda.
“Kila mtu anaweza kutumia kwa mtu ambaye anayo hiyo kitu, nimejaribu kufanya muziki uwe rahisi zaidi na watu waweze kutingisha kichwa” amesisitiza.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi