,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, July 26, 2017

Marehemu enzi za uhai wake.
SIMANZI! Mtoto Nora Jimmy (11), mkazi wa Sinza Mapambano jijini Dar aliyekuwa akisoma darasa la sita Shule ya Msingi Atlas, amedaiwa kufanyiwa kitendo cha kikatili cha kubakwa kisha kunyongwa mpaka kufa na mjomba wake aitwaye John Msigala.
MSIKIE MAMA MZAZI
Akizungumza kwa simanzi kubwa jana, mama wa mtoto huyo, Agness Msigala alisema kuwa siku ya tukio juzi saa 10 jioni yeye hakuwepo nyumbani bali alimuacha mtoto wake huyo na wadogo zake watatu ambao wawili ni wa kiume.Aliongeza kuwa alipotoka kazini alipita kwenda kumuona mgonjwa ambaye ni mama wa rafiki yake lakini alipokuwa anarudi nyumbani, njiani alipigiwa simu na jirani yake na kumueleza kuwa Nora, ameanguka wamempeleka Hospitali ya Palestina hivyo kabla ya kwenda nyumbani apitie hapo. Nilipopigiwa simu hiyo nilishtuka sana na kuanza safari ya kwenda Palestina huku nikiwa na hofu kwa sababu mwanangu nilipoondoka jana yake kwenda kwa baba yake kisha nikaamkia huko kwenda kazini alikuwa yuko vizuri tu.
Wazai wake wakihuzunika.
“Baada ya kufika hospitali nilikutana na jirani yangu pamoja na manesi ambao walijaribu sana kunituliza huku wakinipa moyo wakiniambia kuwa inabidi nijikaze kwani mtoto wangu tayari ameshafariki dunia.“Nilichanganyikiwa na nikaomba nikahakikishe, niliruhusiwa na nilipomchunguza vizuri niliona amefanyiwa kitendo cha ubakaji na pia shingoni kuna alama ya kamba…,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi, ilielezwa kuwa muda mfupi uliopita alizimia.

BABA ANENA
Naye baba mzazi wa mtoto huyo, Jimmy Mariale, alisema kuwa ameumizwa na kifo cha mtoto wake huyo kwa kuwa ndiyo wa pekee na atahakikisha sheria inafuata mkono wake na kama shemeji yake ndiye aliyefanya ukatili huo atahakikisha haki inatendeka.
“Nimeumia mno mtoto wangu ndiye wa pekee sina mwingine kitendo alichofanyiwa ni cha kinyama na kinaumiza mno lakini nitahakikisha sheria inachukua mkondo wake,” alisema baba huyo.
Simanzi ikitawala.
WASIKIE MAJIRANI
Gazeti hili lilizungumza na mmoja wa majirani aliyejitambulisha kwa jina moja la Chacha aliyekuwa eneo la tukio ambaye alisema kuwa akiwa anajiandaa kutoka kwenda kwenye shughuli zake aliona majirani wengi wakiwa nje ya nyumba hiyo huku mwili wa Nora ukiwa umelala chini wakijishauri kuupeleka hospitali.Alipohoji kulikoni aliambiwa kuwa amekutwa amenyongwa pembezoni mwa banda lao la kuku na hata alipoenda kuchunguza sehemu ambayo amekutwa amenyongwa pia aliona panatatanisha.“Mpaka sasa hivi mimi siamini ni kitu gani kimetokea jamani maana sehemu ambayo inadaiwa ndipo aliponyongwa ni fupi mno maana miguu inaweza kugusa chini. Inashangaza sana,” alisema jirani huyo.
IGP Sirro.
WENZAKE WAANGUA KILIO
Baadhi wanafunzi wenzake wa Shule ya Atlas waliompitia mwenzao jana wakiwa kwenye basi la shule waliangua kilio walipokuta mwenzao ameshafariki dunia baada ya kukuta kundi la watu nyumbani hapo, jambo lililozidisha simanzi mtaani hapo.
“Huyu marehemu alikuwa na kawaida ya kuwagongea milango wenzake ili wawahi kupanda basi, hivyo leo hakufanya hivyo na ndiyo maana umewaona wenzake wamemlilia sana,” alisema jirani mwingine.

MJOMBA ASIMULIAMmoja wa mjomba wa marehemu, aliyejitambulisha pia kwa jina la John (ni mtoto wa baba mkubwa na mdogo na mtuhumiwa) ambaye yeye hakuwepo nyumbani hapo tangu asubuhi alisema kuwa kamba ambayo imekutwa shingoni mwa Nora, yeye aliifunga siku tatu za nyuma nyumbani hapo kwa ajili ya kumnyongea paka aliyekuwa akisumbua usiku.Mtuhumiwa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) ambapo afisa mmoja kituoni hapo amethibitisha kukamatwa kwa kijana huyo.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi