,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, August 12, 2017

Image result for Dudu Baya
Msanii Dudu Baya amemkingia kifua msanii Godzilla ambaye hivi karibuni amekuwa akiandamwa sana na msanii Ney wa Mitego akisema muziki umemshinda, na kumtaka Ney kutojifananisha na Godzilla.

Dudu Baya amesema Ney wa Mitego asithubutu kujifananisha na Godzilla kwani hawezi kufikia uwezo wa kuchana kama ambavyo anasema, huku akifananisha uwezo wake kuwa sawa na wasanii kama Gigy Money na Amber Lulu.
"Ney wa mitego sio Mc asiingie kwenye level za kina Godzila, Nash Mc, kwa sababu hana uwezo wa kuandika kama alionao Godzilla, uandishi wa Ney ni sawa na Gigy Money na Amber Lulu", alisema Dudu Baya.
Dudu Baya aliendelea kusema kuwa aina ya nyimbo ambazo anaandika Ney anaweza kuziandika hata mia kwa siku moja, huku akisema kitendo cha Godzilla kukaa kimya ni kitu cha kawaida kwenye muziki.
"Huwezi jua ana mitikikasi gani, kukaa kimya sio kama umeishiwa mashairi, muziki unahitaji kujipanga, promotion, alafu unaanza tour, siwezi kujua ukimwaya wake ni nini lakini najua Godzilla ni mkali", alisema Dudu Baya.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi