,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, August 12, 2017

Msanii mkongwe na miongoni mwa waasisi wa muziki wa bongo fleva Juma Nature, amewajia juu wasanii wa sasa na kuwatuhumu kuwa wanaharibu muziki, huku akiubatiza jina jipya na kuuita miyeyusho.

Juma Nature amesema wasanii wa sasa hivi hakuna cha maana wanachokiimba ukilinganisha na kipindi cha ambacho wao walikuwa wanafanya muziki.
"Muziki wa zamani una maana kuliko wa sasa ninavyohisi mimi, kwa sababu nyimbo za zamani zilikuwa na ujumbe mkali, zinagusa zaidi jamii, watoto wa sasa hivi wanaharibu mziki kwa sababu kila mtu anaimba mapenzi tu, sidhani kama nyimbo za mapenzi zina ujumbe", alisema Juma Nature.
Juma Nature aliendelea kusema kuwa pamoja na kwamba kipindi chao walikuwa wanaimba muziki wa mapenzi, lakini ulikuwa na ujumbe ambao unaishi tofauti na ilivyo sasa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi