,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, August 1, 2017

Mfalme wa kisingeli Tanzania, Msaga Sumu amefunguka kwa kudai hana mpango wa kwenda kuweka meno ya bandia ili kuziba mapengo yaliyopo katika kinywa chake kwa kuwa sasa hivi hicho ndiyo kitambulisho chake cha kumtofautisha na wengine.

Msaga Sumu ameeleza hayo kupitia EATV baada ya kuwepo maoni kutoka kwa baadhi ya mashabiki kumtaka mfalme huyo kuziba mapengo yake kwa kile wanachokiamini sasa hivi anapesa anaweza kubadilisha muonekano wake.
"Walishatokea wadau wakataka kunipeleka nchi ya Ureno kwa ajili ya meno kuwekewa yale yenyewe kabisa kama haya ambayo ninayo lakini mimi mwenyewe nikasema hamna isitoshe watu wengi walishanipiga hela kutumia mimi lakini sasa hivi nikishuka tu sehemu watu wanajua ndiyo mwenyewe kwa sababu ya mapengo yangu", amesema Msaga Sumu.
Kwa upande mwingine, Msaga Sumu amesema hakumbuki mpaka sasa ni meno mangapi yametoka katika kinywa chake kwa kuwa watu wanaotekea pande za Kusini huwa meno yanayotoka wenyewe bila ya kufanya jambo lolote.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi