,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, August 1, 2017

Baba mtoto wa msanii Linah Sanga, Mchomvu amedai picha alizopiga msanii huyo akiwa mjamzito ni za kawaida na kwamba alihusika kwa asilimia zote kuhakikisha zoezi linaenda sawa ikiwa ni pamoja na kuandaa mavazi, ingawa kwa jamii ilionekana tofauti

Aidha ameongeza kuwa picha kama zile kwa Linah ambaye ni mwanamuziki hazina shida hata kidogo ingawa kwa jamii ya kiafrika zilionekana hazina maadili na kuongeza kwamba watanzania wanapenda kuviona vitu hivyo kwa wasanii kutoka nchi za magharibi tu na vikifanyika hapa ndani inakuwa ni uvunjaji wa maadili.
"Mimi kwangu picha zile nilizichukulia kawaida sana kutokana na kazi yake anayoifanya Linah. Linah ni msanii lakini pia alikuwa na furaha ya kupata mtoto.  Mtu wa kawaida akipiga zile picha nitamshangaa hata mimi. Lakini picha hizi hizi wanapiga kina Beyonce, na mashabiki wanataka wasanii wetu wafikie levo zile kwa hiyo watulie ndipo tunapoelekea. Lakini niweke wazi mimi nilihusika asilimia zote ikiwa ni pamoja na yale mafuta ambayo watu walikuwa wanajiuliza nani kampaka. Linah hakuwa anataka mtu mwingine auguse mwili wake ndiyo maana nilikuwa naye karibu kila wakati," alisema
Akizungumzia kuhusu ushirikina kutajwa kama chanzo cha Linah kuchelewa kujifungua, Mchomvu amefunguka na kusema hakuna ushirikina uliohusika kuchelewesha mama mtoto wake kujifungua kwa sababu ya kupiga picha zilizokuwa zikimuonesha sehemu kubwa ya tumbo lake wazi na kutaka watu waelewe ni mambo ya kawaida yanayotokea kwa mama mjamzito.
Picha za Linah zilizozua gumzo mitandaoni wakati wa ujauzito.
Mchomvu ameweka wazi mbele ya kamera za eNewz kupitia EATV na kusema kuwa ni kweli mama mtoto wake alipitiliza wiki tatu baada ya tarehe za makadirio kupita hali ambayo hata Linah ilimtia wasiwasi kidogo na kupelekea kufikiri macho ya watu yamechangia.
"Hakuna ushirikina wowote ambao uliendelea kwa mama mtoto wangu zaidi ni mambo tu ya uzazi ambayo hutokea watu wengi. Linah alipitiliza muda wa kujifungua hadi kufika miezi tisa na wiki tatu hali ambayo ilianza kumtisha na kumfanya awe na wasiwasi labda zile picha alizopiga na kuweka mitandaoni zinazoonyesha tumbo lake. Watu wengine pia walikuwa wakimpa wakati mgumu kwa kumzungumzia, lakini kwa vile siamini sana ushirikina nikawa nampa moyo lakini kiukweli alipata wakati mgumu kwa maneno yaliyokuwa yakizungumzwa." aliongeza
Mbali na hayo  Mchovu amesema jina la mtoto wake kuwa la kizungu sana  (Tracy Paris) alipewa na babu yake mzaa baba ambaye kwa sasa ni marehemu na alitoa hilo jina wiki mbili kabla ya umauti kumfika hali anayoichukulia kama baraka kutoka kwa baba yake.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi